• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wataalamu wa China waisaidia Iraq kupambana na COVID-19

    (GMT+08:00) 2020-03-09 09:19:05

    Timu ya wataalamu saba iliyotumwa na Shirika la Msalaba Mwekundu la China na Kituo cha kinga na udhibiti wa magonjwa cha China imewasili mjini Baghdad kuisaidia Iraq kupambana na maambukizi ya COVID-19.

    Kiongozi wa timu hiyo ya China Bw. Tao Zhongquan amesema China imepata uzoefu katika mapambano dhidi ya ugonjwa huo, na kwamba Iraq itanufaika kutokana na kuzuia, kudhibiti, kugundua na kutibu ugonjwa huo.

    Naibu waziri wa afya wa Iraq Bw. Jasim al-Falahi ameishukuru serikali ya China kwa msaada wake, na kusema China itaimarisha juhudi za kuzuia na kudhibiti maambukizi ya ugonjwa huo nchini Iraq. Kutokana na kuenea kwa ugonjwa huo katika eneo la Mashariki ya Kati, Misri jana iliripoti kifo cha kwanza kutokana na ugonjwa huo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako