• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Umoja wa Afrika wadhamiria kuongeza juhudi kutatua uwiano wa kijinsia Afrika

    (GMT+08:00) 2020-03-09 09:26:12

    Umoja wa Afrika umesisitiza ahadi yake ya kuimarisha juhudi za kutatua uwiano wa kijinsia (gender parity) barani humo, wakati dunia inaadhimisha Siku ya Kimataifa ya Wanawake.

    Kwenye taarifa iliyotolewa jana Jumapili, mwenyekiti wa Kamati ya Umoja wa Afrika Mousa Faki Mahamat amesema umoja huo wenye nchi wanachama 55, unajitahidi kuelekea kutimiza uwiano wa kijinsia na kuhakikisha wanawake na wanaume wanapata fursa sawa.

    Bw. Mahamat amesema Kamati ya Umoja wa Afrika inaheshimu wanawake wa Afrika kutokana na mchango wao kwenye maendeleo na malashi ya bara hilo, na kusisitiza kuwa siku hiyo ni muhimu katika kalenda ya bara hilo na ya kimataifa kwa ajili ya usawa wa kijinsia na uwezeshaji wa wanawake.

    Kwenye mkutano wa 33 wa kilele wa Umoja wa Afrika uliofanyika hivi karibuni mjini Addis Ababa, viongozi wa Afrika waliitangaza miaka kumi ijayo kuanzia 2020 hadi 2030 kuwa Muongo wa Wanawake wa Afrika kuhusu Ushirikishwaji Kifedha na Kiuchumi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako