• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • IGAD yasisitiza ahadi yake kwa haki za wanawake

    (GMT+08:00) 2020-03-09 09:26:27

    Jumuiya ya Maendeleo ya Kiserikali ya Nchi za Afrika Mashariki IGAD imesisitiza ahadi yake kwa haki za wanawake wakati jumuiya ya kimataifa inaadhimisha Siku ya Kimataifa ya Wanawake.

    Kwenye taarifa iliyotolewa jana, Katibu mtendaji wa IGAD Bw. Workneh Gebeyehu amesema IGAD itatumia fursa hii kurejea na kusisitiza dhamira yake ya kulinda, kuhimiza na kutimiza haki za wanawake kupitia hatua zake za kuleta amani, ustawi na mafungamano ya kikanda.

    Bw. Gebeyehu amesema wataongeza juhudi za kuimarisha ustahimilivu wa wanawake wanaoishi kwenye maeneo yaliyoathiriwa na ukame, kuongeza ufuatiliaji kwa wanawake na wasichana wahamiaji na wanawake wakimbizi, kuimarisha ufuatiliaji kwa haki za wanawake kwa ardhi, kupanua ushiriki wa wanawake kwenye ujenzi wa amani na utatuzi wa migogoro kupitia kazi ya usuluhishi kwenye Jukwaa la Wanawake, Amani na Usalama la IGAD.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako