• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Harambee Starlets yapokea kichapo cha 5-0 dhidi ya Chile

    (GMT+08:00) 2020-03-09 10:03:32

    Harambee Starlets imekubali kichapo katika mechi yake ya pili ya soka ya kimataifa ya Turkish Women's Cup baada ya kuaibishwa 5-0 na Chile katika mechi ya Kundi B iliyogaragazwa Jumamosi uwanjani Gold City mjini Alanya nchini Uturuki. Mabingwa wa Afrika Mashariki na Kati (Cecafa) walikuwa wameichapa Northern Ireland 2-0 katika mechi yao ya ufunguzi Machi 4. Chile iliingia mchuano huu ikipigiwa upatu kunga'ara, hasa kwa sababu inaorodheshwa katika nafasi ya 36 kwenye viwango bora vya Shirikisho la Soka Duniani (Fifa). Kenya, ambayo itamenyana na Black Queens ya Ghana katika mechi yake ya mwisho ya makundi Machi 10, ipo katika nafasi ya 133 duniani. Starlets ya kocha David Ouma inatumia mashindano haya ya timu nane kujipiga msasa kabla ya kuvaana na Tanzania katika mechi yake ya raundi ya kwanza ya kutafuta tiketi ya kushiriki Kombe la Bara Afrika (AWCON) baadaye mwaka 2020. Kenya na Tanzania zitapepetana mwezi Aprili, huku mshindi akikutana na mshindi wa mechi nyingine ya raundi ya kwanza kati ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na Sao Tome & Principe katika raundi ya pili ili kuingia AWCON 2020.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako