• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Simba wawa vibondo wa Yanga wanyukwa 1-0

    (GMT+08:00) 2020-03-09 10:04:06

    Bernard Morrison, kiungo mshambuliaji wa Yanga jana ametenda kazi yake iliyompelekea Bongo kwa kuifunga Simba bao 1-0 kwenye mchezo wa mzunguko wa pili uliochezwa Uwanja wa Taifa. Bao pekee la ushindi lilifungwa dakika ya 44 kwa mpira wa adhabu alioupiga kiungo huyo raia wa Ghana na kuuzamisha mzima langoni baada ya Aishi Manula kuzidiwa nguvu na mpira huo. Mpaka dakika 90 zinakamilka Simba ya Meddie Kagere ilishindwa kufurukuta mbele ya Yanga waliokuwa wakifanya mashambulizi ya hatari huku nyota wa mchezo kwa Yanga akiwa ni Metacha Mnata ambaye aliokoa michomo mingi ya hatari kwa Simba iliyokuwa ikipigwa na Meddie Kagere. Ushindi huo unaifanya Yanga kufikisha pointi 50 ikiwa imecheza mechi 25 huku Simba ikiwa na pointi 68 imecheza mechi 27 za Ligi Kuu Bara

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako