• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: City yasalimu tena amri kwa mara ya pili Old Trafford yalimwa 2-0

    (GMT+08:00) 2020-03-09 10:06:47

    Bao la Anthony Martial katika awamu ya kwanza na la Scott McTominay dakika ya lala salama yaliweka pengo kubwa huku Man United wakipata ushindi mara mbili dhidi ya Man City wakati wa kivumbi cha Manchester derby. Mechi hiyo iliyochezwa jana usiku ilimshuhudia Martial akiandikisha historia katika uwanja wa Old Trafford huku akiibuka mchezaji wa pili wa United kufunga mabao mfululizo katika gozi la Ligi Kuu dhidi ya Manchester baada ya Eric Cantona. Huku wakipata ungwaji mkono mkubwa katika uga ya nyumbani Old Trafford, Mashetani Wekundu walianza awamu ya kwanza ya debi hiyo kwa ari ya juu huku wakitengeneza nafasi nyingi za mabao. Martial na Dan James walikabidhiwa wajibu mkubwa na kujaribu kufungua ukurasa wa mabao bila kufaulu. Hatimaye wenyeji walipenya kuwa kifua mbele kupitia kwa Martial ambaye alimalizia vyema mpira wa adhabu wa Bruno Ferndandes. Mabadiliko yaliyomshirikisha Riyad Mahrez na Gabriel Jesus yalikosa kuleta matokeo huku dakika tano za nyongeza zikiwa baraka kwa United ambao walipachika bao lao la pili kupitia kwa McTominay ambaye alitumia vyema masihara ya goli kipa Ederson. Vijana wa Ole Gunnar Solskjaer kwa sasa wamekamilisha ligi kwa kuikabithi City kichapo cha pili kwa mara ya kwanza tangu uongozi wa kocha mstaafu Sir Alex Ferguson. Ushindi huo uliwapandisha wenyeji hao wa Old Trafford hadi katika nafasi ya tano kwenye jedwali na pointi 45 ambapo ni tofauti ya pointi tatu pekee nyuma ya Chelsea ambao waliwaponda Everton 4-0.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako