• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Sudan yazihimiza Misri na Ethiopia zirejeshe mazungumzo juu ya Bwawa la Nile

    (GMT+08:00) 2020-03-09 10:22:41

    Wizara ya mambo ya nje ya Sudan imetoa taarifa ikizihimiza Misri na Ethiopia zirudi kwenye meza ya mazungumo, na kufikia makubaliano juu ya Bwawa la GERD la Ethiopia.

    Taarifa hiyo inatoa wito kwa Misri na Ethiopia zisichukue hatua zinazoweza kutoa athari hasi kwa mchakato wa mazungumzo, pia inasisitiza tena kwamba Sudan inataka kufanikisha mazungumzo ya GRED ili kuhakikisha maslahi ya nchi hizo tatu.

    Taarifa imeongeza kuwa Sudan haijakubali rasimu ya azimio iliyotolewa na Baraza la mambo ya nje katika Jumuiya ya Nchi za Kiarabu tarehe 4 mwezi huu, kwa kuwa Sudan haikushirikishwa kwenye utungaji wa rasimu hiyo, ambayo inaona haiendani na madhumuni ya mazungumzo yanayoendelea sasa.

    Tarehe 29 mwezi Februari, Misri ilisaini makubaliano kuhusu utekelezaji wa GERD yaliyoandaliwa na Marekani bila kushirikiwa na Ethiopia. Ethiopia imepinga makubaliano hayo na kutoa wito wa kutohimiza mchakato wa GERD kabla ya pande tatu husika kufikia mwafaka.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako