• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kituo cha polisi magharibi mwa Cameroon chashambuliwa

    (GMT+08:00) 2020-03-09 10:22:57

    Habari kutoka jeshi la usalama la Cameroon zimethibitisha kuwa wapiganaji wasiojulikana wameshambulia kituo cha polisi kilichoko wilayani Galim magharibi mwa nchi hiyo tarehe 7 usiku, ambako watu wasiopungua watano wameuawa.

    Habari zinasema waasi hao takriban 20 walifanya shambulizi wakiwa wamepanda pikipiki, na kuwaua polisi wawili, askari wawili na mtu mmoja aliyefungwa, na polisi wengine wanne wamejeruhiwa.

    Waasi hao pia walipora baadhi ya silaha na mabomu kutoka kituo cha polisi. Hadi sasa, hakuna kundi lolote au mtu yeyote aliyetangaza kuhusika na shambulizi hilo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako