• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ufaransa yapiga marufuku mikusanyiko ya watu zaidi ya 1,000 kutokana na kuongezeka kwa maambukizi ya COVID-19

    (GMT+08:00) 2020-03-09 10:23:48

    Waziri wa afya wa Ufaransa Bw. Olivier Veran ametangaza kuwa, Ufaransa itapiga marufuku kwa muda mikusanyiko ya umma inayoshirikisha watu zaidi ya 1,000, wakati zaidi ya watu 1,000 wamegunduliwa kuambukizwa virusi vya korona nchini humo.

    amesema shughuli zote zinazotarajiwa kuwavutia zaidi ya watu 1,000 zitapigwa marufuku nchini kote, isipokuwa zile zinazothibitishwa kuwa na "umuhimu kwa maisha ya raia".

    Serikali ya Ufaransa hapo awali ilikuwa imepiga marufuku mikusanyiko yote ya watu 5,000 katika maeneo yaliyofungwa, na pia shughuli kadhaa katika mazingira ya wazi nchini kote. Pia leo waziri huyo amesaini amri ya kurashisha upatikanaji wa huduma za matibabu kwa njia ya mawasiliano ya simu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako