• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Shirika la ndege la Ethiopia launga mkono juhudi za China za kupambana na COVID-19 kwa vitendo

    (GMT+08:00) 2020-03-09 17:02:12

    Shirika la ndege la Ethiopia limepongezwa kwa kuwa shirika la ndege la nchi za nje lililofanya safari nyingi zaidi na kupeleka abiria wengi na vifaa vingi zaidi za kinga kwa China wakati wa mlipuko wa ugonjwa wa virusi vipya vya korona COVID.

    Ethiopia inafuatilia na kuunga mkono juhudi za China za kupambana na maambukizi ya COVID-19, na kupongeza China kwa kila maendeleo iliyoipata.

    Mkurugenzi Mkuu wa Shirika hilo Tewolde Gebremariam amesema, kusimamisha safari za ndege na kutoa vizuizi vya utalii si utatuzi, bali ushirikiano unasaidia kinga na udhibiti wa maambukizi hayo.

    Ndani ya mwezi mmoja, shirika hilo limefanya safari nyingi za ndege za mizigo, pia limechukua hatua mbalimbali za kuanzisha njia za haraka na kusafirisha abiria na mizigo kwa pamoja, ili kuhakikisha kwa ufanisi usafiri wa vifaa vya uokoaji wa China.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako