• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Idadi ya maambukizi ya COVID-19 nchini Misri yafikia 55

    (GMT+08:00) 2020-03-09 19:04:15

    Misri imetangaza kuwa kesi saba mpya zimethibitisha kuwa maambukizi ya COVID-19 ndani ya nchi hiyo, na kufanya idadi ya jumla ya watu waliothibitishwa kuwa na maambukizi hayo kufikia 55.

    Msemaji wa Wizara ya Afya nchini Misri Khaled Megahed amesema, kesi saba mpya ni pamoja na raia wanne wa kigeni na Wamisri watatu, mmoja kati yao akitokea Saudi Arabia baada ya kufanya hija ndogo, na wawili waliwasiliana moja kwa moja na raia wa Misri aliyerejea nchini humo hivi karibuni akitokea Serbia.

    Jana, Misri iliripoti kifo cha kwanza kutokana na maambukizi ya virusi vipya vya korona, ambapo mtalii mmoja raia wa Ujerumani mwenye umri wa miaka 60 aliwasili nchini humo siku saba zilizopita alipelekwa kwenye hospitali ya hoteli ya Red Sea iliyoko Hurghada.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako