• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • WHO yajitahidi kuhakikisha nchi za Afrika zinagundua kesi ya kwanza ya COVID-19

    (GMT+08:00) 2020-03-09 19:13:15

    Ofisa wa Shirika la Afya Duniani WHO barani Afrika Mary Stephen amesema, jukumu la kwanza kwa Afrika katika kukabiliana na ugonjwa wa nimonia inayosababishwa na virusi vipya vya Korona (COVID-19) ni kuhakikisha kuwa nchi zote zinaweza kugundua kesi ya kwanza ili kuzuia kuenea kwa virusi hivyo.

    Stephen amesema, hadi sasa nchi 27 za Afrika zina uwezo wa kupima na kugundua COVID-19, na nchi nyingi za bara hilo zimeanzisha vituo vya dharura vya afya ya umma na taratibu husika za uratibu na pia kutunga mipango ya kitaifa ya kukabiliana na virusi hivyo.

    Hadi Jumapili, nchi 9 za Afrika zimethibitisha kesi za COVID-19 ambako wagonjwa wote waliambukizwa virusi kabla ya kuingia katika nchi hizo.

    Hata hivyo Stephen ameonya kuwa, kadri nchi nyingi zinavyokumbwa na ugonjwa huo, ndivyo hatari ya wasafiri wa nchi za Afrika kuingiza virusi katika nchi zao inavyoongezeka.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako