• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yaikosoa Marekani kwa kukashifu juhudi zake za kupambana na COVID-19

    (GMT+08:00) 2020-03-09 19:13:42

    China imemkosoa waziri wa mambo ya nje wa Marekani Mike Pompeo kwa kukashifu juhudi zake za kutoa taarifa kwa uwazi kwa jamii ya kimataifa kuhusiana na ugonjwa wa nimonia inayosababishwa na virusi vipya vya korona COVID-19

    Hivi karibuni, Pompeo alisema Marekani imechelewa kuchukua hatua kupambana na COVID-19 kwa sababu haikupata taarifa kamili kutoka China

    Akizungumzia hilo, msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Geng Shuang amesema, baada ya kulipuka kwa COVID-19, China imekuwa ikitoa taarifa kwa uwazi na uwajibika kwa Shirika la Afya Duniani WHO na nchi na sehemu mbalimbali duniani ikiwemo Marekani, kueleza mpangilio wa vinasaba vya virusi, kujibu ufuatiliaji wa pande mbalimbali na kuimarisha ushirikiano wa kimataifa, juhudi ambazo zimetambuliwa na kupongezwa na jamii ya kimataifa.

    Kuhusu Pompeo kuviita virusi vya korona kuwa "virusi vya Wuhan", msemaji huyo amesema WHO imetoa jina rasmi la virusi vya korona, na Pompeo hakuheshimu sayansi wala uamuzi wa WHO, na kufanya kila awezalo kuchafua China na Wuhan kwa kutumia virusi vya korona na China inalaani kitendo hiki kiovu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako