• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya Rais atoa agizo la kuongezeka kwa bei ya mpunga kutoka Sh45 hadi Sh85.

    (GMT+08:00) 2020-03-09 19:16:53

    Wakulima wa mpunga katika Mpango wa Unyunyuzaji maji wa Kano Magharibi wamehimizwa kupeleka mpunga wao kwa bodi moja ya Unyunyuzaji maji ili kupata bei nzuri.

    Meneja wa mpango huo Joel Tanui amesema wakulima wanapaswa kutii agizo la rais ili waepuke kuuza mazao yao kwa madalali kwa bei ya kutupa

    Aidha ameambia wakulima kuwa bei itaendelea kuboreka na wakati, Rais Uhuru Kenyatta ametoa wito wa kuongezeka kwa bei ya mpunga kutoka Sh45 hadi Sh85.

    Wakati huo huo, meneja amesema kuwa mipango inaendelea ya upanuzi wa skimu ya umwagiliaji Kano Magharibi kutoka ekari 11,000 ya sasa hadi 16,000.

    Upanuzi huo unatarajiwa kuendana na kuongezeka kwa idadi ya mchele unaovunwa.

    Mwezi uliopita, Kenyatta aliamuru Wizara ya Kilimo kuongeza bei ya mchele kufuatia malalamiko kutoka kwa wakulima.

    Rais amesema serikali yake imejipanga kuhakikisha kwamba wakulima hawateseka tena kutokana na ukosefu wa soko la mazao yao.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako