• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mwanadiplomasia wa China asema hakuna nafasi ya ubaguzi katika vita ya dunia dhidi ya COVID-19

    (GMT+08:00) 2020-03-09 19:23:17

    Balozi mdogo wa China ofisi ya ubalozi mjini Los Angeles, Marekani, Zhang Ping amesema wakati dunia inajitahidi kudhibiti kuenea kwa virusi vipya vya korona, watu wanatakiwa kujilinda dhidi ya kuenea kwa virusi vya kisiasa na kibaguzi.

    Katika maoni yake yaliyochapishwa kwenye gazeti la Los Angeles Times, mwanadiplomasia huyo amesema kumekuwa na ripoti za kutatiza duniani kuhusu kutengwa na kubaguliwa kwa jamii ya Wachina. Amesema licha ya majibu yake ya makini dhidi ya janga hilo, serikali ya China imeshambuliwa na baadhi ya watu kutokana na nadharia za upendeleo. Balozi Zhang amesema, kutokana na mlipuko wa ghafla wa virusi hivyo visivyojulikana, serikali ya China ilichukua hatua kali na za kina za afya ya jamii ambazo hazijawahi kuchukuliwa katika mlipuko wowote, kwa lengo la kupata matokeo chanya. Ameongeza kuwa, hatua zilizochukuliwa na China hazikuwa tu kwa manufaa ya watu wake wenyewe. Kwa kuweka hatua kali na za nguvu ndani ya nchi na kushirikiana kwa karibu na jamii ya kimataifa, ikiwemo Shirika la Afya Duniani (WHO), China ilitumika kama mstari wa nguvu wa kulinda kuenea kwa kasi kwa janga hilo, na kutoa nafasi muhimu kwa nchi nyingine kuimarisha hatua za maandalizi dhidi ya mlipuko huo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako