• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China kuimarisha hatua za kuzuia virusi vipya vya korona kutoka na kuingia nchini

    (GMT+08:00) 2020-03-09 20:50:29

    China itaimarisha hatua za kupambana na virusi vipya vya korona katika forodha, ikiwa ni juhudi za kuzuia virusi hivyo kutoka na kuingia nchini humo.

    Hayo yamebainishwa leo hapa Beijing katika mkutano wa kukabiliana na maambukizi ya virusi vipya vya korona ulioendeshwa na waziri mkuu wa China Li Keqiang. Mkutano huo umesema ili kukabiliana na changamoto mpya zinazotokana na kuenea kwa kasi kwa maambukizi mapya ya virusi hivyo nje ya nchi, China inatakiwa kuimarisha ushirikiano wa kimataifa na kushughulia vizuri kazi za kusimamia afya za wasafiri wanaotoka au kuingia nchini humo, hatua itakayolinda usalama wa watu wanaosafiri kati ya nchi. Mkutano huo pia umesema watu wanaoingia China wakiwa wamethibitishwa au kushukiwa kuambukizwa virusi hivyo na wale wanaowasiliana na wagonjwa wanatakiwa kufuata hatua za kupimwa, kutibiwa, kuwekwa karantini au kuangaliwa afya zao.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako