• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • WHO: asilimia 70 ya walioambukizwa COVID-19 nchini China wamepona

    (GMT+08:00) 2020-03-10 09:00:25

    Mkurugenzi mkuu wa Shirika la Afya Duniani WHO Bw. Tedros Ghebreyesus amesema zaidi ya asilimia 70 ya watu elfu 80 walioambukizwa COVID-19 nchini China wamepona na kuondoka hospitali, hali inayoonesha kuwa China imefanikiwa kudhibiti mlipuko wa ugonjwa huo.

    Bw. Tedros amesema katika mkutano wa kila siku kuwa maambukizi ya virusi vya korona yanaweza kupunguzwa na kudhibitiwa kupitia hatua za haraka na za mapema, na kutoa wito kwa nchi zote kufuata mkakati kamili wa kukabiliana na mlipuko wa COVID-19 na kushinda mapambano dhidi ya virusi vya korona.

    Kwa mujibu wa ripoti ya kila siku ya WHO, hadi kufikia jana jumatatu, maambukizi karibu laki 1.1 yamethibitishwa kote duniani, na maambukizi 3,994 yaliongezeka kwa siku, 3,949 yakiwa nje ya China.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako