Kamati ya kitaifa ya mawaziri ya kukabiliana na maambukizi ya COVID-19 nchini Ethiopia, imetangaza hatua mbalimbali za kuzuia mlipuko wa COVID-19 nchini humo.
Kamati hiyo iliyoundwa wiki iliyopita kwa ajili ya kufuatilia kwa karibu juhudi zinazoendelea za kuzuia mlipuko wa COVID-19 nchini humo, imemwarifu Waziri Mkuu wa Ethiopia Bw. Abiy Ahmed kuhusu juhudi zinazoendelea za kuitayarisha nchi hiyo dhidi ya maambukizi ya COVID-19.
Kwa mujibu wa kamati hiyo, kwa kushirikiana na mashirika mengine husika, wizara ya afya ya Ethiopia imeanzisha kituo cha dharura cha saa 24 cha kukabiliana na maambukizi ya COVID-19, wakati huo huo, upimaji kwa wasafiri wote wanaoingia nchini kupitia ardhi na anga pia unaendelea.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |