• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Aston Villa yaendelea kufanya vibaya EPL yachapwa 4-0 na Leicester City

    (GMT+08:00) 2020-03-10 10:08:21

    Memneja wa Leicester City Brendan Rodgers amesema timu imefanya vizuri huku Jamie Vardy akimaliza ukame wa magoli walipowarambisha sakafu Aston Villa kwa 4-0. Mbweha hao wamepata ushindi mara mbili katika mechi zao nane za Ligi ya Premier na pointi 4 katika mechi zao nne za nyuma. Nyota wa mechi hiyo Harvey Barnes ndiye aliyetangulia kuliona lango la Aston Villa na kufunga bao la uongozi katika dakika ya 40 na pia kufunga bao la kumalizia dakika ya 85. Naye Vardy pia alichana wavu wa Aston Villa mara mbili katika dakika ya 63 na bao la penalti dakika ya 79. Kwa matokeo hayo, Aston Villa ya Dean Smith ipo kwenye eneo la hatari kushushwa daraja baada ya kushindwa mara nne mfululizo kwenye ligi, na mara tano kwenye mashindano yote. Aston Villa ipo katika nafasi ya 19 ya msimamo wa EPL ikiwa na pointi 25. Kabla ya mtanange huo ocha Mkuu wa Aston Villa, Dean Smith alizungumzia juu ya kiwango cha Samatta tangu alipojiunga na klabu hiyo kwenye dirisha dogo la usajili la Januari mwaka huu. Smith amemtaja Samatta kuwa ni kijana mwenye akili kubwa ambaye ataisaidia klabu hiyo katika wakati huu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako