• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Mo Dewji ataka Simba na Yanga zikutane tena katika Kombe la FA

    (GMT+08:00) 2020-03-10 10:09:13

    Mwenyekiti wa Bodi ya Simba, Mohamed Dewji 'Mo' bado hajakubali matokeo ya kipigo ilichopata timu yake kutoka kwa Yanga akiomba wakutana tena katika Kombe la FA. Simba imefungwa bao 1-0 na Yanga katika mchezo wa pili wa Ligi Kuu uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa, shukrani kwa bao pekee la Bernard Morrison. Baada ya kipigo hicho MO Dewji jana kupitia ukurasa wake wa Twitter aliweka picha inayoonyesha takwimu za mchezo wa Yanga na Simba na kuandika 'Hongereni Sana wana Yanga. Mungu akitujalia tutakutana kwenye FA.' Hii ni wazi kwamba MO Dewji na mashabiki wengi wa Simba bado hawajakubali na kipigo walichopata kutoka kwa watani zao Yanga juzi. Mapema jana Afisa Habari wa Simba, Haji Manara mtu aliyetaniwa zaidi na Wanayanga kwa kutumia picha zake mbalimbali, lakini kupitia ukurasa wake wa Instagram aliipongeza Yanga kwa ushindi. Manara aliandika "Wanasimba wenzangu niwape salaam zangu fupi za kuwaomba kwanza tukubali tumepoteza mchezo kwa kufungwa na timu iliyocheza vizuri kuliko siye, na tukubali hilo halibadiliki kwa sasa, najua tumeumia ila hiyo ndiyo footbali tuliyoichagua kuipenda. "Kwa tamaduni zetu lazima tucharurwe kama ambavyo tungewacharura iwapo tungeshinda, but life goes on, Muhimu kujipanga kwa mchezo unaofuata keshokutwa, tusitoke ktk reli na sote tunajua ubingwa upo mikononi mwetu, tusithubutu kumtafuta mchawi wala kulaumiana. Wametufunga kihalali kabisa na ni haki yao kutamba!! Alimaliza kuandika ujumbe wake Manara

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako