• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mwenyekiti wa tume ya AU alaani vikali shambulizi dhidi ya waziri mkuu wa Sudan

    (GMT+08:00) 2020-03-10 10:24:44

    Taarifa iliyotolewa na Umoja wa Afrika imesema mwenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika Bw. Moussa Faki Mahamat amelaani vikali shambulizi dhidi ya msafara wa magari wa waziri mkuu wa Sudan Bw. Abdalla Hamdok mjini Khartoum.

    Habari zinasema Bw. Hamdok amenusurika kifo kufuatia msafara wake wa magari kushambuliwa kwa mabomu yaliyotegwa kwenye gari katika eneo la kuingia kwenye daraja la jeshi la Sudan.

    Umoja wa Afrika umewahimiza wadau wote walinde mshikamano wa serikali ya mpito ya Sudan, na kulinda matokeo ya demokrasia. Bw. Mahamat pia ametoa wito kwa wadau husika kudumisha matokeo mapya yaliyopatikana nchini Sudan.

    Wakati huohuo, baraza la usalama na ulinzi la Sudan limelaani shambulizi dhidi ya waziri mkuu Bw. Abdalla Hamdok, tukio ambalo ni kitendo haramu, na kuonyesha hatari inayoikabili Sudan kutoka ndani, kwa upande wa kikanda na wa kimataifa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako