• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tz: Mfumuko wa bei wathibitiwa

    (GMT+08:00) 2020-03-10 18:12:54

    Mfumuko wa bei kwa mwezi Februari mwaka huu umebakia kuwa asilimia 3.7 kama ilivyokuwa kwa Januari ya mwaka huu.

    Akizungumza na waandishi wa habari hapo jana, kaimu mkurugenzi wa sensa ya Watu na Takwimu za Jamii kutoka ofisi ya Taifa ya Takwimu, Ruth Minja, alibainisha kuwa kasi ya mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma kwa mwaka ulioisha, Februari mwaka huu imebaki kuwa sawa na kasi iliyokuwepo kwa mwaka ulioisha Januari 2020.

    Hatua hiyo imechangiwa na kuongezeka na kupungua kwa bei za bidhaa zikilinganishwa na bei za Februari mwaka jana.

    Bi Minja pia aligusia hali ya mfumuko wa bei ya bidhaa kwa baadhi ya nchi za Afrika Mashariki kwa mwaka ulioishia Februari 2020, ambapo alibainisha kuwa Kenya, mfumuko wa bei umeongezeka hadi asilimia 6.37 kutoka asilimia 5.78 kwa mwaka ulioishia Januari 2020.

    Nchini Uganda, mfumuko wa bei kwa mwaka ulioishia Februari mwaka huu, umebakia kuwa asilimia 3.4, kama ilivyokuwa kwa mwaka ulioishia Januari, 2020.

    Mfumuko wa bei wa taifa unapimwa kiwango cha kasi ya mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma zote zinazotumiwa na kaya binafsi nchini.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako