• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uganda: Bidhaa kutoka China zapungua

    (GMT+08:00) 2020-03-10 18:13:20

    Bidhaa kutoka China zimepungua mno kutokana na mlipuko wa virusi vya corona nchini China.Kufikia sasa, Uganda imeshuhudia upungufu wa bilioni 6 kutokana na hali hii, baada ya China ambalo ni taifa la pili ulimwenguni kwa ukuaji wa uchumi kukumbwa na virusi vya cirina ambavyo vimeathiri shughuli za biashara za mataifa mengi.

    Mwezi Desemba mwaka jana, Uganda ilitumia dola milioni 109.82 kwa kununua bidhaa kutoka China. Kwa sasa, bajeti hiyo imepungua hadi dola milioni 108.14. Wachanganuzi wa masuala ya uchumi na biashara wanakisia kwamba hali huenda ikawa mbaya zaidi endapo virusi hivi vya corona vitazidi kuenea. Kando na hilo, thamani ya shilingi ya Uganda imepungua kutoka na hali hii.

    Kwa miaka mingi, China imekuwa mshirika mkuu wa biashara na Uganda, huku bidhaa nyingi zinazouzwa nchini humo zikitoka China.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako