• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya: Hatutaki maziwa duni.

    (GMT+08:00) 2020-03-10 18:13:42

    Kenya imetoa ilani kali kwamba haitaruhusu maziwa yasiyo ya kiwango bora kuingia kwenye soko lake. Haiya ni kwa mujibu wa waziri wa Kilimo Peter Munya, ambaye anasema kwamba kuna mikakati kabambe ya kuwalinda wafugaji ng'ombe wa maziwa nchini Kenya, ili kuhakikisha kwamba wanafaidika kutokana na biashara ya maziwa yao. Aidha, waziri Munya anasema kwamba serikali iko mbioni kufufua sekta ya maziwa kitaifa , na hivyo hawataruhusu maziwa kutoka mataifa ya nje.

    Kumekuwepo na vuta nikuvute kati ya Kenyua na Uganda kuhusiana na swala zima la maziwa. Kenya imekuwa ikizuia maziwa na bidhaa zote za maziwa kutoka Uganda kuingia nchini Kenya. Baadhi ya maziwa ya Uganda ambayo yamekuwa yakiuzwa nchini Kenya ni yale ya Lato na Lakeside Dairy.

    Ikizingatiwa kuwa matumizi ya maziwa yako chini sana nchini Uganda, wafanyibiashara wa bidhaa hiyo walikuwa wamepata soko zuri nchini Kenya ila sasa, wanazidi kukadiria hasara baada ya agizo la waziri Munya.

    Kwa wakati fulani, malori ya 30 yaliyokuwa yamebeba maziwa kutoka Uganda kwenda Kenya, yalifungiwa kuingia na kulazimika kurejea Uganda.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako