• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Burkina Faso yathibitisha wagonjwa walioambukizwa virusi vipya vya Korona kwa mara ya kwanza

    (GMT+08:00) 2020-03-10 18:56:44

    Burkina Faso imethibitisha kwa mara ya kwanza kuwa watu wawili wameambukizwa virusi vipya vya korona, na hadi kufikia sasa, nchi sita zilizoko kusini mwa Sahara barani Afrika zimeripoti maambukizi ya virusi hivyo.

    Waziri wa afya wa Burkina Faso Bibi Claudine Lougue amesema, watu wawili waliothibitishwa kuambukizwa virusi vya korona ni wachumba, na mwanamke aliwahi kwenda nchini Ufaransa. Hivi sasa wagonjwa hao wanaendelea kupata matibabu, na mtu mwingine aliye karibu na wagonjwa hao ametengwa na anafanyiwa uchunguzi.

    Wakati huohuo, Waziri wa afya nchini Afrika Kusini Dr Zwelini Mkhize amesema, watu wanne zaidi wameambukizwa virusi vipya vya korona na kwa ujumla watu 7 wamethibitishwa kuambukizwa virusi hivyo nchini Afrika Kusini.  

    Nchini Nigeria, Wizara ya afya nchini humo imethibitisha mtu wa pili kuwa na maambukizi ya virusi vya korona na kufanya idadi ya watu wenye maambukizi hayo kufikia wawili. Wagonjwa hao wanaendelea vizuri.

    Ripoti ya kila siku ya maambukizi ya virusi vya korona inayotolewa na Shirika la Afya Duniani (WHO) imeonyesha kuwa, hadi kufikia jana, kulikuwa na wagonjwa wanne nchini Senegal, wagonjwa wawili nchini Cameroon na mgonjwa mmoja nchini Togo, na hakuna kesi mpya kwenye nchi hizo tatu katika saa 24 zilizopita.  

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako