• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uganda kugawa neti milioni 27 katika mapamano mapya dhidi ya malaria

    (GMT+08:00) 2020-03-10 19:01:09

    Wizara ya afya nchini Uganda imesema itagawa neti milioni 27 za mbu mwezi ujao, ikiwa ni katika mapambano mapya dhidi ya ugonjwa wa Malaria, ambao ni moja ya magonjwa yanayoua watu wengi zaidi nchini humo.

    Taarifa iliyotolewa leo na wizara hiyo imesema, wizara hiyo inataka kuhakikisha kuwa wananchi wote nchini humo wanalala chini ya neti zenye dawa kila usiku ili kuzuia malaria, ugonjwa unaosababisha vifo vya watu kati ya elfu 70 na laki moja kila mwaka nchini humo, wengi wakiwa mama wajawazito na watoto wadogo.

    Uganda imepata mafanikio dhahiri katika kupambana na Malaria, huku idadi ya wagonjwa ikipungua kutoka asilimia 19 hadi asilimia 9.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako