• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yapongeza nchi na watu wa Afrika kwa kuunga mkono juhudi zake za kupambana na COVID-19

    (GMT+08:00) 2020-03-10 19:26:22

    China imepongeza nchi na watu wa Afrika kwa kuwa pamoja nayo katika mapambano dhidi ya ugonjwa wa virusi vipya vya korona (COVID-19).

    Jumuiya ya Maendeleo ya kusini mwa Afrika (SADC) jana ilifanya mkutano wa mawaziri wa afya nchini Tanzania, ikisifu na kuunga mkono juhudi za China za kukabiliana na COVID-19 na kusema itaimarisha ushirikiano na uratibu na China.

    Akizungumzia hili, msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Geng Shuang amesema, serikali ya China na watu wake wamejitahidi kupambana na maambukizi hayo na sasa ufanisi umeonekana katika juhudi hizo. Viongozi wa nchi karibu zote zenye uhusiano wa kibalozi na China na mwenyekiti wa Kamati ya Umoja wa Afrika wametoa salamu kwa China, na hata nchi zilizo nyuma kimaendeleo zilitoa misaada ya fedha na vitu kwa China, jambo ambalo linaigusa sana China.

    Geng amesema hatua hizo zimeonesha jinsi China na Afrika zinavyosaidiana kupambana na taabu kama ndugu, na kuwa jumuiya yenye hatma ya pamoja iliyo ya karibu zaidi kati yao. Ameongeza kuwa, hivi sasa nchi za Afrika zinakabiliwa na hatari kubwa ya kuingia kwa virusi vipya vya korona, na China inapenda kutoa misaada kwa nchi hizo kadri inavyoweza na kulinda kwa pamoja usalama wa afya ya umma ya kikanda na kimataifa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako