• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Madaktari wa China wapongezwa kwa kuwaelimisha watu wa Zambia kuhusu COVID-19

    (GMT+08:00) 2020-03-10 19:27:29

    Watu wa Zambia wamewapongeza madaktari wa China kwa kutoa ahadi kushiriki mpango wa kutoa elimu kuhusu virusi vipya vya korona nchini humo.

    Pongezi hizo zimekuja baada ya madaktari wa China kutangaza Jumamosi kuwa wako tayari kuchangia mpango wa kutoa elimu kuhusu virusi hivyo.

    Mdau wa afya kutoka Chingola, Mwangala Mubiana amesema, wamefurahi kuwa wenzao wa China wana hamu ya kuchangia mpango huo, na ahadi zao za kuwa walinzi na kushiriki katika kikosi cha kutoa elimu nchini Zambia ni maendeleo mazuri. Ametoa wito kwa wafanyakazi wengine wa afya waliopo nchini humo kujifunza kutoka kwa wachina hao.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako