• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa China aapa kushinda COVID-19

    (GMT+08:00) 2020-03-10 19:36:58

    Rais Xi Jinping wa China ameapa kupata ushindi katika vita dhidi ya virusi vipya vya korona (COVID-19).

    Rais Xi ametoa ahadi hiyo wakati wa ziara ya ukaguzi aliyoifanya leo katika mji wa Wuhan, mkoani Hubei, ambako kesi ya kwanza ya maambukizi ya virusi vya korona iligunduliwa.

    Rais Xi ameagiza kufanya juhudi thabiti, zenye nguvu na za pande zote kuzuia na kudhibiti virusi, ili kulinda Hubei na Wuhan. Rais Xi ametoa salamu na shukrani kwa wakazi na wafanyakazi walio mstari wa mbele katika kupambana na virusi hivyo baada ya kutembelea wakazi waliowekwa kwenye karantini katika nyumba zao mjini Wuhan, na kukagua kazi ya kuzuia na kudhibiti maambukizi ya virusi vipya vya korona katika Hospitali ya Huoshenshan. Amesema mwelekeo mzuri wa kuzuia na kudhibiti ugonjwa huo uliopatikana hivi sasa usingetimizwa bila ya kujitolea mhanga kwa watu wa Wuhan.

    Aidha, rais Xi pia ametembelea na kutoa salamu kwa wahudumu wa afya, wanajeshi, wafanyakazi wa makazi, askari polisi, viongozi wa serikali za mitaa, watumishi wa serikali za ngazi za juu, watu wanaojitolea, wagonjwa na wakazi mbalimbali.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako