• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania yafuta mkutano wa Baraza la Mawaziri wa SADC kutokana na maambukizi ya COVID-19

    (GMT+08:00) 2020-03-10 19:58:26

    Serikali ya Tanzania imetangaza kufuta mkutano wa Baraza la Mawaziri la Jumuiya ya Uchumi ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) uliopangwa kufanyika kwa siku mbili kuanzia jumatatu ijayo, ikiwa ni maandalizi ya kukabiliana na mlipuko wa virusi vipya vya korona.

    Katibu mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Bw. Wilbert Ibuge amesema, kufutwa kwa mkutano huo kunafuatia mapendekezo yaliyotolewa jana katika mkutano maalum wa mawaziri wa afya wa SADC.

    Mawaziri hao wamependekeza kuahirishwa kwa muda kwa mikutano ya moja kwa moja ya SADC, na kupendekeza kutumia teknolojia za kisasa, ikiwemo mikutano kwa njia ya video na Skype mpaka virusi hivyo vitakapodhibitiwa.

    Ibuge amesema, kuahirishwa kwa mikutano hiyo kunadhamiria kuwalinda wajumbe na maambukizi ya virusi vya korona vinavyoenea kwa kasi sehemu mbalimbali duniani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako