• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais Xi Jinping asisitiza kuimarisha ulinzi wa kimfumo kwa ajili ya kuhakikisha usalama na afya ya wananchi

    (GMT+08:00) 2020-03-11 09:10:02

    Rais Xi Jinping wa China jana Jumanne aliwasili mjini Wuhan kwenye ukaguzi wa kazi ya kudhibiti mlipuko wa virusi vya korona. Rais Xi amesisitiza kuwa udhibiti wa mlipuko huo wa ugonjwa wa COVID-19 ni mtihani mkuu kwa mfumo na uwezo wa usimamizi, na kwamba China inapaswa kutupia macho siku za mbele, kujumuisha uzoefu na kuondoa dosari zilizopo kwenye mfumo wa usimamizi, ili kuimarisha ulinzi wa kimfumo kwa ajili ya kuhakikisha usalama na afya ya wananchi.

    Rais Xi ametoa shukrani zake kwa watu wa Wuhan kutokana na kujitolea na uvumilivu wao, na kusema kutokana na mchango wao mwelekeo mzuri wa leo ndio umeweza kupatikana kwenye mapambano dhidi ya virusi vya korona. Amesema watu wa Wuhan ni shupavu, na wameonesha kivitendo moyo wa watu wa China kujali na kusaidiana katika wakati mgumu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako