• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mtaalamu wa Kenya apongeza hatua madhubuti za China katika kudhibiti mlipuko wa COVID-19

    (GMT+08:00) 2020-03-11 09:10:47

    Mtaalamu wa magonjwa ya kuambukiza wa Kenya amesema hatua zinazochukuliwa na China ambazo zimepunguza maambukizi ya nimonia inayosababishwa na virusi vipya vya korona COVID-19 nchini humo, zinapaswa kuigwa na nchi zote duniani.

    Bw. Rodney Adam, profesa wa patholojia na udaktari na mwenyekiti wa Kamati ya Udhibiti wa Maambukizi katika Chuo kikuu cha Aga Khan cha Nairobi, ameipongeza serikali ya China kwa kuchukua hatua madhubuti za kudhibiti mlipuko wa virusi vya korona.

    Akizungumza kwenye mkutano uliofanyika Nairobi kuhusu COVID-19 na athari zake kwa afya ya umma nchini Kenya, profesa Adam amesema kuchukuliwa kwa haraka kwa hatua zenye ufanisi kama vile kuwaweka kwenye karantini wanaoshukiwa kuambukiziwa, kujenga hospitali za muda na kuhamasisha mwitikio wa pamoja wa wananchi, zimefanikisha juhudi za China kwenye mapambano dhidi ya mlipuko wa virusi vya korona ambao umetajwa kuwa dharura ya kimataifa ya afya ya umma.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako