• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Waziri wa utalii wa Misri asema utalii wa nchi hiyo haitaathiriwa na COVID-19

    (GMT+08:00) 2020-03-11 10:30:58

    Waziri wa utalii wa Misri Khaled al-Anany amesema sekta ya utalii ya Misri haitaathiriwa na COVID-19, na hakuna vituo vyovyote vya utalii vilivyofungwa kutokana na virusi hivyo.

    Bw. Anany amesema katika mwezi wa Februari mwaka huu wakati wa mlipuko wa virusi vya korona, watalii karibu 900,000 walitembelea Misri, na idadi hiyo iliongezeka kwa asilimia 4 kuliko mwaka jana wakati kama huu.

    Ameongeza kuwa zaidi ya watalii 210,000 walitembelea Misri kwenye wiki ya kwanza ya mwezi Machi mwaka huu, na kuitaja idadi hii kuwa ni "kiwango cha kawaida".

    Vilevile amesema wizara ya utalii inafanya ushirikiano wa karibu na wizara ya afya pamoja na mamlaka nyingine, ili kuwalinda wafanyakazi wa vituo vya utalii na watalii wa ndani na nje.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako