• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Chama cha mashirika ya ndege cha Afrika chatoa wito wa kutekeleza sera za nje ili kulinda mashirika ya kitaifa

    (GMT+08:00) 2020-03-11 10:31:24

    Katibu mkuu wa Chama cha mashirika ya ndege cha Afrika AFRAA Bw. Abderahmane Berthe ametoa wito wa kuchukua sera ya nje ya kibara ili kuyalinda mashirika ya ndege ya kitaifa dhidi ya ushindani wa kimataifa.

    Bw. Berthe amesema hivi sasa nafasi ya soko la mashirika ya ndege ya Afrika imeshuka hadi kufikia asilimia 20 ya uchukuzi wa abiria kati ya Afrika na nchi nyingine duniani. Ili kubadilisha hali hii, Afrika inahitaji sera ya anga ya nje ya ngazi ya Umoja wa Afrika. Ameongeza kuwa Umoja wa Ulaya vilevile una sera kama hiyo ambayo inalinda mashirika yake ya ndege katika ushindani wa kimataifa.

    Bw. Berthe pia amesema mlipuko wa virusi vya korona umeathiri sekta ya usafiri wa anga barani Afrika kutokana na kusimamishwa na kufutwa kwa safari nyingi za ndege.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako