Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa FAO limekabidhi magari kumi kwa Kenya ili kuisaidia kunyunyiza dawa za kuulia nzige wa jangwani.
Waziri wa kilimo wa Kenya Bw. Peter Munya amesema, magari hayo yatapelekwa katika maeneo yaliyoathiriwa vibaya zaidi na nzige wa jangwani ambao wamevamia nchi kadhaa za Afrika Mashariki.
Pia amesema timu ya tathmini itakwenda huko kukagua kiwango cha uharibifu, na kuziwezesha familia zilizoathirika kupewa msaada ili kuwarejesha katika maisha ya kawaida.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |