• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • MBIO ZA BOTI: Mzanzibari ashiriki mbio za boti duniani

    (GMT+08:00) 2020-03-11 10:35:59

    Mashindano ya kuzunguka dunia baharini kwa kutumia boti zinazotumia upepo (Tanga) yamefikia Mjini Subic nchini Ufilipino yakitokea Visiwa vya Papua New Guinea ikiwa ni muendelezo wa mashindano hayo. Kwa mujibu wa AyoTV mshiriki huyo kutoka Zanzibar/Tanzania Nassor El Mahruki amesema matarajio ya kufika katika Mji huo ilikuwa ni kutumia siku tisa isipokuwa kutokana na hali ya bahari kuwa mbaya imewalazimu kutumia siku kumi na moja. Amesema katika safari hii hakukuwa na matukio ya kutisha mbali ya changamoto ndogondogo zilizojitokeza ikiwa ni pamoja na kuchanika kwa matanga kwa baadhi ya boti. El Mahruki amesemea mbali ya kukosekana kwa matukio ya kutisha katika safari yao hiyo ila washiriki watatu katika boti yao wameshindwa kuendelea na mashindano hayo na kutangaza kujiondoa katika mashindano hayo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako