• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • OLIMPIKI: Mwenge wa Olimpiki kukosa shamrashamra kwasababu ya korona

    (GMT+08:00) 2020-03-11 10:36:16

    Kamati ya Olimpiki ya Ugiriki imetangaza kuwa Sherehe ya kuwasha mwenge wa Olimpiki kwa ajili ya michezo ya Olimpiki ya Tokyo inayofanyika majira haya ya joto itafanyika bila ya watazamaji kutokana na mlipuko wa virusi vya korona. Ikitoa tangazo hilo Jumatatu, kamati imesema kwamba wageni muhimu 100 tu kutoka Kamati ya Olimpiki ya Kimataifa na kamati ya maandalizi ya Olimpiki ya Tokyo ndio watakaoruhusiwa kushiriki sherehe hiyo inayofanyika kesho Alhamis huko Olympia, kulikokuwa ikifanyika michezo ya jadi. Mazoezi ya mavazi yanayofanyoka leo pia hayataruhusiwa kwa umma. Mwenge wa Yokyo 2020 umepangwa kuwashwa pamoja na sherehe ya jadi ambayo itafuatiwa na kukimbiza mwenge nchini Ugiriki, na baadaye kukabidhiwa waandaji wa Tokyo kwenye sherehe nyingine itakayofanyika Machi 19 katika uwanja wa Panathenaic huko Athens. Kwenye taarifa yake Tokyo imesema, itajitahidi kupunguza wageni wake kadiri iwezavyo. Mwenge huo nchini Ugiriki utakimbizwa katika miji 37 na maeneo 15 ya kisiwa, ambayo yatachukua kilomita 3,500 na utabebwa na wakimbiaji 600.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako