• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Rwanda yajitoa fainali za CHAN 2020 nchini Cameroon kwasababu ya korona

    (GMT+08:00) 2020-03-11 10:36:31

    Serikali ya Rwanda imeamua kuchukua tahadhari mapema kuhusiana na mlipuko wa virusi vya korona ambavyo vimeingia katika baadhi ya nchi. Rwanda imeamua na kufikia maamuzi ya kutangaza kutoshiriki fainali za CHAN 2020 nchini Cameroon zinazotarajiwa kuanza April 4 2020 lakini pia na mechi za kuwania kufuzu AFCON 2021. Fainali hizo za Cameroon zinatia hofu kutokana na nchi hiyo tayari hadi kufikia March 9 walikuwa wameripotiwa wagonjwa wawili wa korona kubainika. Wakati huohuo Afisa habari wa shirikisho la soka Tanzania TFF Clifford Mario Ndimbo kwa niaba ya kocha mkuu wa timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars Etienne Ndairagije ametangaza kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars chenye majina ya wachezaji 35 ambao watacheza mchezo wa kuwania kufuzu AFCON 2021 na fainali za CHAN zitakazofanyika April nchini Cameroon, Kapombe na Abdi Banda waitwa Taifa Stars.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako