• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Tottenham Hotspurs nje ya michuano ya ligi ya Mabingwa

    (GMT+08:00) 2020-03-11 10:36:45

    Klabu ya Tottenham Hotspurs inayofundishwa na kocha wake Jose Mourinho jana usiku iliaga rasmi michuano ya UEFA Champions League msimu wa 2019/20 kwa kuondolewa na RB Leipzig, licha ya msimu uliopita kufika hadi hatua ya fainali. Mourinho na vijana wake walikuwa ugenini lakini walienda kutafuta ushindi kwa kuwa mchezo wa kwanza nyumbani kwao London walipoteza mchezo huo kwa kufungwa goli 1-0. Mechi ya marudiano imekuwa mbaya zaidi kwa Mourinho kwa kujikuta akipoteza mchezo wa pili kwa kufungwa kwa magoli 3-0, magoli ya RB Leizig yakifungwa na Marcel Sabtzer aliyefunga mawili dakika ya 10 na 21 na mwisho likafungwa na Emil Forsberg dakika ya 87.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako