• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Mbao yajiweka pabaya Ligi Kuu

    (GMT+08:00) 2020-03-11 16:42:10

    Wakati Azam FC ikipata ushindi dhidi ya Ruvu Shooting, Mbao FC imezidi kujiweka katika nafasi finyu ya kubaki katika Ligi Kuu Tanzania Bara kwa msimu ujao. Mchezo kati ya Mbeya City na Mbao FC ulizikutanisha timu hizo ambazo zote zinapigania nafasi ya kubaki kwenye ligi kuu na kuepuka kushushwa daraja katika msimu ujao. Katika mechi hiyo, Mbao FC walifungwa bao 1 – 0 na Mbeya City katika mchezo uliochezwa Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya. Matokeo hayo yameifanya Mbeya City kufikisha point 30 huku Mbao wakiwa na point 22. Wakati huohuo, timu ya soka ya Black Sailors kule Unguja imeendelea kujiimarisha kileleni mwa msimamo wa Ligi Daraja la Kwanza Kanda ya Unguja baada ya kuifunga Mchangani United bao 1 – 0 katika mechi iliyochezwa Uwanja wa Mao Zedong na kufikisha point 34.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako