• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Ndayiragije Aita Wachezaji 35 wa Taifa Stars

    (GMT+08:00) 2020-03-11 16:42:27

    Kocha mkuu wa timu ya soka ya taifa Tanzania (Taifa Stars), Etienne Ndayiragije, ametaja kikosi cha wachezaji 35 watakaojiandaa na mechi ya kuwania kufuzu AFCON 2021 dhidi ya Tunisia na michuano ya CHAN 2020. Kikosi hicho kitaingia kambini kesho kwa ajili ya maandalizi ya mchezo utakaochezwa Machi 27 nchini Tunisia na kurudiana tarehe 30, Machi 2020 jijini Dar es Salaam. Baadhi ya wachezaji wanaounda kikosi hicho ni pamoja na Mbwana Samatta anayechezea timu ya Aston Villa nchini Uingereza, Nickson Kibabage wa timu ya Diffa El Jadid ya Morocco, na Farid Mussa anayekipiga CD Tenerife kule Hispania.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako