• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Idadi ya kesi za maambukizi ya COVID-19 barani Afrika yapita 100

    (GMT+08:00) 2020-03-11 17:54:11

    Mkurugenzi wa Kituo cha Kukinga na Kudhibiti Magonjwa cha Afrika CDC Bw. John Nkengasong amesema, idadi ya kesi za maambukizi ya ugonjwa wa nimonia inayosababishwa na virusi vipya vya korona (COVID-19) imepita 100 na mtu mmoja amefariki kutokana na maambukizi hayo.

    Bw. Nkengasong amesema, kituo hicho kimepeleka wataalam 6 katika nchi za Nigeria na Cameroon kusaidia kupambana na virusi hivyo, na mpaka sasa, nchi 43 za Afrika zina uwezo wa kupima virusi hivyo.

    Bw. Nkengasong pia amesema, kituo hicho kinashirikiana na Shirika la Afya Duniani kutoa vifaa vya upimaji wa virusi hivyo kwa nchi za Afrika na kuharakisha kununua vifaa vya kupima joto ya mwili na vifaa vingine vya matibabu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako