• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Msomi wa Kenya asema, ziara ya rais wa China mjini Wuhan imeonyesha imani ya China kushinda maambukizi ya COVID-19

    (GMT+08:00) 2020-03-11 17:55:09

    Mkuu wa taasisi ya sera za Afrika ya Kenya Bw. Peter Kagwanja amesema ziara ya rais Xi Jinping wa China ya kukagua kazi ya kupambana na virusi vipya vya korona mjini Wuhan, mkoa wa Hubei imeonesha imani ya China kushinda mapambano dhidi ya virusi hivyo.

    Akihojiwa na Shirika Kuu la Utangazaji la China (CMG), Bw. Kagwanja anasema,

    Kitendo cha rais Xi kwenda mji wa Wuhan kufanya ukaguzi ni kama tangazo la China la kukaribia kushinda mapambano dhidi ya virusi vya korona. Ingawa bado kuna masuala kadhaa yanayohitaji kutatuliwa, kitendo hicho kimetilia moyo watu wanaofuatilia sana hali ya China.

    Hivi sasa, COVID-19 imeenea katika nchi zaidi ya 100. Bw. Kagwanja anasema, serikali ya China imechukua hatua sahihi kudhibiti maambukizi ya ugonjwa huo ambazo si tu zimeiletea matumaini kwa China bali pia jamii ya kimataifa. Pia amesema, uzoefu uliopatikana na Afrika kutoka China ni kwamba ni lazima kuchukua hatua yenye ufanisi ya kuzuia na kudhibiti mapema maambukizi.

    "Hatua yenye ufanisi ya kuzuia na ya kudhibiti virusi ni uzoefu tuliojifunza kutoka China. Ingawa bado hatuna dawa ya kutibu ugonjwa huo, lakini tunaweza kushinda kwenye mapambano hayo. Tunaona fahari kwa jitihada zilizofanywa na Wachina katika mapambano hayo. "

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako