• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yasema kukata mnyororo wa uzalishaji na utoaji si kitendo cha busara

    (GMT+08:00) 2020-03-11 17:56:49

    Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Geng Shuang amesema, wakati dunia inakabiliana na maambukizi virusi vipya vya korona COVID-19, kukata mnyororo wa kimataifa wa uzalishaji na utoaji wa bidhaa si kitendo cha busara, na pia hakitafanikiwa.

    Geng amesema athari ya maambukizi ya ugonjwa huo kwa uchumi wa China ni ya muda mfupi, na inadhibitika. Amesema China ina mfumo kamili zaidi wa uzalishaji duniani, na jumuiya ya kimataifa ina matarajio mazuri kuhusu uwezo wa China katika kukabiliana na changamoto za sekta za uzalishaji na utoaji nchini humo.

    Ameongeza kuwa katika zama ya utandawazi, maslahi ya nchi mbalimbali yanaungana kwa kina, na mnyororo wa uzalishaji na utoaji wa bidhaa duniani umeunganisha kila nchi. Wakati dunia inakabiliana na maambukizi ya virusi, jaribio la kukata mnyororo huo, au kudai kutenganisha uhusiano wa kiuchumi, si kitendo cha busara.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako