• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ajira zanukia kiwanda cha ngozi

    (GMT+08:00) 2020-03-11 19:34:55

    Mkuu wa Gereza la Karanga lililopo Wilaya ya Moshi mkoani Kilimanjaro, Rajab Igongi, ameweka wazi kuwa ajira za kiwanda cha bidhaa za ngozi kinachojengwa na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), kwa ubia na jeshi hilo zitahusisha wataalamu mbalimbali ambao si askari.

    Igongi aliyasema hayo juzi, wakati Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Dk. Anna Mghwira na kamati yake ya ulinzi na usalama walipotembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa kiwanda hicho kipya cha kwanza nchini.

    Ujenzi wa kiwanda hicho utagharimu, zaidi ya Sh. bilioni 75.3 na unatarajia kukamilika mwezi Februari mwaka huu na ujio wake utafungua fursa za ajira kwa watu zaidi ya 4,000.

    Akiwa katika eneo la ujenzi wa mradi huo, Mkuu wa Mkoa huo, Dk. Mghwira alipata fursa ya kuzungumza na uongozi wa Gereza la Karanga pamoja na kutembelea majengo mbalimbali yanayojengwa katika eneo hilo la mradi.

    Igongi alisisitiza kuwa kiwanda hicho kitakapoanza kazi kitachangia mapato kwa kuwa mamlaka mbalimbali za kukusanya mapato zitakusanya kodi kutokana na uzalishaji wa kiwanda hicho.

    Mradi huo ulianza mwezi Oktoba, mwaka jana na ulitarajiwa kukamilika Machi, mwaka huu.

    Kulingana na takwimu za Wizara ya Mifugo, ngozi ghafi inayotokana na mazao ya mifugo, zaidi ya vipande milioni nane huwa vinapotea, kati ya vipande milioni 10 vinavyozalishwa nchini.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako