• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mashirika ya ndege na viwanja vya ndege barani Afrika vyachukua hatua kukabiliana na COVID-19

    (GMT+08:00) 2020-03-12 09:15:09

    Shirika la ndege la Msumbiji LAM limetangaza kuwa litapunguza safari za ndege za ndani kutokana na kupungua kwa kiasi kikubwa kwa abiria kufuatia mlipuko wa nimonia ya COVID-19 inayosababishwa na virusi vya korona.

    Shirika la ndege la Algeria Air Algerie pia limetangaza siku hiyohiyo kusimamisha safari zake za ndege kwenda mji wa Rome hadi Aprili 15 kutokana na mlipuko wa COVID-19 unaokithiri nchini Italia.

    Bunge la Zimbabwe limesema uwanja wa ndege wa kimataifa wa Robert Gabriel Mugabe mjini Harare ambao ni uwanja mkubwa zaidi wa ndege nchini humo unahitaji kuimarisha maandalizi dhidi ya mlipuko wa ugonjwa wa COVID-19, ambao mpaka sasa bado hakuna maambukizi yaliyoripotiwa nchini humo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako