• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yathibitisha hatua mpya za kudumisha biashara ya nje na uwekezaji wa nje

    (GMT+08:00) 2020-03-12 09:56:35

    Waziri mkuu wa China Bw. Li Keqiang jana aliitisha mkutano wa Baraza la serikali, na kuthibitisha hatua mpya za kukabiliana na athari za mlipuko wa virusi vya korona, na kudumisha biashara ya nje na uwekezaji kutoka nje, kuondoa vizuizi kwenye minyororo ya viwanda na minyororo ya mitaji, kuhimiza ushirikiano wa pande mbalimbali kwa ajili ya kurejesha uzalishaji mali, kutekeleza vizuri sera ya mikopo maalumu, ili kuhakikisha ugavi wa bidhaa muhimu na kuyasaidia makampuni kupitia wakati huu mgumu.

    Mkutano huo umesisitiza kuwa, China lazima ishikilie kufungua mlango zaidi kwa nje. China itarudisha kodi kwa wakati kwa bidhaa zinazouzwa kwa nje ambazo zinafikia vigezo, kuongoza benki kuongeza mikopo kwa biashara ya nje, na kupanua orodha ya Sekta zinazoruhusiwa kuwekezwa na wawekezaji wa nje.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako