• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Cecafa yapata Mtendaji Mkuu mpya baada ya Nicholas Musonye kuachia ngazi

    (GMT+08:00) 2020-03-12 10:10:31

    Baraza la Vyama vya Mpira wa Miguu Afrika Mashariki na Kati (Cecafa) limemtangaza Auko Gacheo kuwa Mtendaji Mkuu (CEO) mpya akimrithi Nicholas Musonye aliyemaliza muda wake. Musonye amekabidhi rasmi utawala wake kwa Meneja wa zamani wa SuperSport Afrika Mashariki Auka Gacheo kwenye hafla iliyofanyika jana Jumatano katika ofisi za Shirikisho la Soka Tanzania zilizopo jijini Dar es Salaam. Hivi karibuni Musonye alitangaza nia ya kujiunga na siasa na amesema sasa yuko tayari kwa kipindi chake kingine cha maisha yake. Mwenyekiti wa Cecafa, Wallace Karia amemshukuru Musonye kwa huduma yake kwenye shirikisho hilo na baadaye kusema Gacheo amekidhi vigezo walivyoviweka hadi kupewa nafasi hiyo. Akizungumza na waandishi wa habari, Gacheo alisema kuwa anafahamu kazi ngumu aliyonayo ya kuleta maendeleo ya soka Afrika Mashariki na Kati.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako