• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Liverpool yatupwa nje ya Ligi ya Mabingwa baada ya kupigwa 3-2 na Atletico Madrid

    (GMT+08:00) 2020-03-12 10:11:06

    Mabingwa watetezi wa Ligi ya Mabingwa jana usiku walikabwa koo na Atletico Madrid baada ya kumaliza mechi ya marejeano hatua ya 16 bora na kuchabangwa 3-2. Vijana wa Jurgen Klopp walikuwa wanataka kushinda kombe kwa mara ya saba wakidhani wataweza kugeuza matokeo ya awali ambayo walishindwa na Atletico 1-0 katika uwanja wa Wanda Metropolitano, Uhispania. Goli la kichwa la Georginio Wijnaldum katika dakika ya 43 kipindi cha kwanza lilikuza matumaini ya Liverpool. Hata hivyo vijana wa Klopp waliendelea kusaka magoli na kufanikiwa tena kutingisha wavu katika dakika ya 94 lililofungwa na Firmino. Nayo Atletico Madrid ilianza kucharuka kwenye dakika ya 97 na kuanza kuimiminia mvua ya magoli Liverpool. Na hadi kipenga cha mwisho kinalia Liverpool ililazwa chali kwa 3-2.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako