• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kilele cha mlipuko wa virusi vya korona nchini China kimepita

    (GMT+08:00) 2020-03-12 16:57:19

    Msemaji wa Kamati ya Afya ya China Bw. Mi Feng amesema, kilele cha mlipuko wa virusi vya korona nchini China kimepita.

    Bw. Mi amesema, idadi ya kesi mpya za maambukizi ya virusi hivyo inaendelea kupungua, kwamba Machi 11 (jana), kesi 8 mpya ziliripotiwa mjini Wuhan, ambao ni mji mkuu wa mkoa wa Hubei ulioathiriwa vibaya zaidi na maambukizi. Na kesi nyingine 7 mpya zimeripotiwa katika China bara licha ya mkoa wa Hubei, miongoni mwao, 6 ni wagonjwa walioambukizwa nje ya China.

    Maendeleo hayo yamekuja wakati Shirika la Afya Duniani (WHO) likitangaza kuwa mlipuko wa virusi vya korona unaweza kuchukuliwa kama janga, kwa kuwa virusi hivyo vinaendelea kuenea kwa kasi duniani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako